“Wizara
inapenda kutamka kwamba kitendo cha Balozi yoyote kuhudhuria mikutano
ya hadhara ya vyama vya siasa na kuvaa sare zenye nembo ya vyama vya
siasa siyo sahihi na kinakiuka Kifungu cha 41(1) cha Mkataba wa
Vienna wa mwaka 1961, unaoongoza uhusiano wa kidiplomasia,” alisema
Membe katika taarifa yake jana jioni.
Taarifa
hiyo ilisema kuwa mkataba huo unazuia wawakilishi wa nchi za nje
kujihusisha na ushabiki wa kisiasa wanapofanya kazi zao kwenye nchi
za uwakilishi.
“Katika
kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012, Wizara ilikumbana na vitendo
vinavyofanana na kitendo hiki na ikachukua hatua stahiki, kadhalika
kwa tukio hili Wizara itachukua hatua za kidiplomasia zinazostahili
ili kuzuia jambo hili lisitokee tena,” alisisitiza.
Taarifa
hiyo ilisema kuwa Balozi huyo alikwenda wilayani humo kuhudhuria
uzinduzi wa mradi wa viwanda vya kuchambulia pamba vinavyojengwa na
mwekezaji wa Kichina anayeitwa Tahong, na viwanda hivyo vitakuwa na
uwezo wa kuchambua tani 120,000 za pamba kwa mwaka, vitakapokamilika
mwakani.
Alisema
Wizara imeona picha na habari kwenye vyombo vya habari zikieleza na
kumuonyesha Balozi huyo akiwa kwenye mkutano wa CCM.







0 comments:
Post a Comment