Wasanii wa muziki wa bongo fleva kutoka katika kundi la Tanzania House of talent THT wakatazwa kuimba na kufanya onesho katika mgahawa wa nyumbani lounge unaomilikiwa na msaani nguli wa bongo fleva lady jaaydee.
Inadaiwa kuwa kiongozi wa THT ambae pia ni kiongozi wa juu katika Radio CLOUDS FM Luge Mutahaba ndie aliewakataza wasanii walio chini yake kufanya onesho lolote lile katika ukumbi uliopo katika mgahawa huo unaomilikiwa na J DeeAkifunguka katika ukurasa wake wa tweeter mwanadada lady jaydee amewataja wasanii kama Lina sanga na Ben paul kuwa walizuiliwa kufanya tamasha hilo siku ya valentine day February 14 mwaka huu licha ya kuwa teyari walishapokea pesa nusu kwa ajiri ya kufanya onesho hilo.
“Wasanii wa THT walikatazwa kuja kuimba Nyumbani Lounge siku ya Valentine na boss wao. Mbali na kuwa walishalipwa hela za advance
Linah na Ben Pol mnabisha hamkukatazwa? Nisalitini ila hamtapata faida mtatoka kapa pia”
kiongozi huyo
alifanya hivyo akidhani kuwa Lady Jaydee ndie alieandaa show hiyo
kumbe yeye alitoa tu ukumbi kwa mtu mwingine kama ambavyo anafunga
sasa“Walidhani ni show yangu, wakafikiri nitatajirika. Ila nilitoa ukumbi tu wakamsaliti alieandaa show. Not me”
sakata la hili la JayDee kufunguka juu ya watu wanaoitwa mahalamia wa muziki bongo limefuatia siku kadhaa baada ya watu hao kutumia nguvu zao nyingi na pesa zao kuhalibu kazi za wasanii,tukumbuke watu hao na Radio hiyo alianza kulalamikiwa kwanza na Dudubaya na kuja na project aliipa jina la MANGURUWE akiwa na maana kuwa watu hao si wazuri kwani wanaua muziki wa kibongo.
Baadae akaja Mh mbunge wa mbeya Mr 2 na kuwalalamikia watu hao hao na Redio hiyohiyo Clouds media mpaka wakaja na project inayokwenda kwa jina la ANT VIRUS iliyokuwa na lengo la kuwaonesha watanzania kuwa kuna watu wachache nchini wanaoua muziki wa kibongo akiwemo kiongozi huyo na Redio hiyo hiyo kutokana na ukweli huo wasanii waliunganisha nguvu na kujiita vinega waliokuwa na wanaopinga na kupigana na mahalamia hawa wa muziki
na leo hii mwanadada Ladyjaydee ambae alikuwa karibu sana na watu hao ameanza kufunguka ya moyono kuwa watu hao na Redio hiyo wanauwa muziki wa kitanzania na kuwanyonya wasanii wa muziki wa kibongo hii ni wazi kuwa shutuma hizo sio uzushi wala longo longo bali ni kitu ambacho kipo.







0 comments:
Post a Comment