7:22 AM
Kwa siku kadhaa tumeshuhudia
wabunge wakirushiana maneno ya kifedhuli sana lakini nje ya Bunge
wanaitana 'mambo vipi kaka' 'sema ndugu yangu' nk.
Jibu
ni rahisi sana. Kwanza, Siasa za Tanzania zimejengwa kwenye misingi
ya UNAFIKI. Ushabiki huzaa unafiki, hivyo watu wanapotaka shabikia
kitu hujikuta wanafanya unafiki ili kuonekana wao ni mashabiki zaidi.
Pili,
kuna siasa za kujipendekeza kwa wakubwa ili wakubwa waone kuwa 'duh
huyu jembe huyu, anatetea sana msimamo wa chama'. Binaadamu wengine
wameumbwa hivyo na hivyo ni lazima kukubaliana na hali hiyo na kisha
kuweka mikakati ya ku 'manage' hali hiyo.
Tufanyeje?
@Filikunjombe kasema 'CCM ijikite kwenye kutimiza ahadi zake kwa
wananchi ili wapinzani wakose cha kusema' inaweza kuwa hatua
mojawapo.
Lakini
kwa vyovyote CHADEMA hatutakosa cha kusema kwani kuna mambo mengi
sana ya kusimamia ili kuhakikisha kuwa wananchi wanafaidi kodi yao.
Suluhisho
la kudumu ni kujenga vikundi vya kibunge vilivyo juu ya vyama vya
siasa na vyenye maslahi kwa Umma. Kwa mfano mpango wa kuanzisha 'Oil
and Gas Parliamentary Caucus' unapaswa kuharakishwa ili wabunge wawe
na masuala ya kufanyia kazi na kuzungumza katika nyakati za ku
'socialise'. 'Parliamentary Education Caucus' nayo hivi sasa ni kama
inachungulia kaburi. Wabunge wapenda soka na wapenzi wa Taifa Stars
tuna kundi la Parliamentarians for TaifaStars, makundi kama haya
yanapaswa kudumishwa ili kuwaweka Wabunge katika mahusiano ya
kitaaluma badala ya mahusiano ya kunywa na kucheza disco tu.
Mahusiano
ya Wabunge ya kitaaluma yatamaliza malumbano ya hovyo bungeni na
kuruhusu wabunge kuwa na muda wa kutosha kujadiliana kwa hoja na
kuisimamia Serikali iwajibike.
Tatizo
kubwa Tanzania ni Uwajibikaji. Uwajibikaji ndio suluhisho la UFISADI
nchini. Uwajibikaji utapelekea utajiri wa nchi kutumika kuondoa
umasikini.Uwajibikaji utaondoa malumbano ya hovyo hovyo Bungeni.
0 comments:
Post a Comment