9:43 PM

NG’OMBE – TAURUS
(APR21 – MAY 20)
Mipango yako kabambe uliyoipanga inaweza
ikageuka ikawa balaa au vurugu na unatakiwa usiwe mgumu katika
kubadili mipango hiyo inapobidi.Kama itakuwa unasisitiza kutobadilika
basi itakuwa ni kuvurugika kwa mambo yako yote.
MAPACHA -
GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Utapata nafasi ya kukutana na viongozi
wako, itumie vizuri nafasi hiyo kuweka sawa mambo yako ya kimaisha.
Elewa kwamba sayari ya Jupiter itakuwa katika nyota yako kwa muda wa
miezi kadhaa na hiyo inaashiria kupata safari za ghafla za hapa na
pale. Jitahidi kutumia nafasi hiyo kujinufaisha.
.
KAA -
CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo itakuwa siku nzito kwako, inamaanisha
hata mambo yako na matamanio yako yatakuwa mazito kwa hiyo usijaribu
kufanya lolote, Jaribu kutumia wakati huu kuwa na familia yako kwa
matembezi hasa wakati wa jioni.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG
22)
Utapata furaha ya kurudishwa kazini au katika biashara au
mpenzi wako kurudi. Kama uko kazini jaribu kumalizia kazi
zinazokukabili na usijaribu kukwaruzana na wafanyakazi wenzio. Elewa
kwamba hao unaofanya nao kazi wamekuchoka kama wewe
ulivyowachoka.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kama kaka
yako au dada yako anataka kuzungumza habari nyeti na wewe tafadhali
kwa njia yoyote ile msikilize, lakini jaribu kuficha mawazo yako.
Jambo lolote ambalo utaliamua leo unaweza kulibadili hapo baadae.
Jitayarishe kwa majaribu.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Weka masikio yako wazi, kuna mtu utapata habari zake na anaweza
kukusaidia kupata fedha. Wakati huu Sayari za Mwezi na Uranus
zinatembelea nyota yako na ndio wakati wako wa kupata fedha. Fanya
mipango ya Fedha sasa na zungumza na watu wenye fedha utapewa
Mkopo.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Jaribu kutekeleza
majukumu yako yote leo kabla jua halijazama. Nyota haziwezi kukupa
nafasi katika kipindi kinachokuja. Utaona kwamba mipango mingi
itakwama na watu hawatokupa msaada unaohitaji. Ni vyema ukawa kivyako
katika muda wa wiki moja mpaka balaa hilo liondoke.
MSHALE -
SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Jaribu kuwa mtulivu kama mpenzi
wako au mshirika wako au mmoja wa watu ndani ya famila yako
akidhamiria kukuacha.Ni kweli watakuwa na sababu nzito za kufanya
hayo lakini njia watakazozichukua haziridhishi. Hivi sasa utahitaji
sana kutumia busara ili kuepusha migongano.
MBUZI - CAPRICORN
(DES 22 – JAN 20)
Hali ya wasiwasi inayokukabili bado ipo.
Inaonekana kuwa wewe ni mtu unayependa sana amani na unataka sana
kufanya Amani. Pamoja na kwamba utahisi kwamba juhudi zako
hazithaminiwi utapata faraja mwisho wa siku baada ya mchango wako
kuthaminiwa.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Sayari
ya Venus inaingia kwenye nyota yako wiki ijayo na hiyo ni dalili ya
kunyooka kwa mambo yako ya kimapenzi. Kipindi hiki itakuia urahisi
sana kupata mpenzi mpya au kutengeneza tena uhusiano ambao umevunjika
kati yako na mkeo au mpenzi wako.
SAMAKI – PISCES (FEB 20-
MACH 20)
Leo utapata majukumu mengi ya nyumbani. Jaribu kutumia
uwezo wako wa ushawishi kuwafanya wengine waone dhamira yako. Fanya
kazi zako kutoka nyumbani. Tafuta mipango mipya na biashara mpya ili
uweze kuvutia wateja wa aina nyingine.
PUNDA- ARIES (MACH 21-
APR 20)
Mawazo yako hivi sasa ni kusafiri na unafanya kila njia
kushirikisha watu ili safari hiyo ifanikiwe. Safari ipo na itakuwa.
Leo jioni hutopata uzito wa kumpata mtu wa kuwa nae katika kipindi
hicho. Utatfutwa kusuluhisha ugomvi wa rafiki yako kuwa tayari
kumtetea.
0 comments:
Post a Comment