Wednesday, May 8, 2013

HATUTAFUTA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE-NECTA


Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza  Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Prof Mkandala ameweka wazi msimamo wake huo kama mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa na kusema kuwa haoni haja na tija kufuta matokeo ya kidato cha NNE ya mwaka 2012 kwa kuwa waliptisha Matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao hivyo haoni sababu ya kufuta matokeo hayo na hata kama yanafutwa ni kwa faida ya nani na kwa ustawi ya Elimu ya wapi? Alihoji Prof. Mkandala

'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' 

Kutokana na sakata linaloendelea nchini sasa juu ya matokeo ya kidato cha nne na msimamo wa serikali kuhusiana na kufuta matokeo ya kidato cha Nne na kutaka kusahihishwa upya,Mwenyekiti na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachioa ngazi ikitokea Serikali ikisimamia msimamo wake ho wa kufuta matokeo ya Kidato cha Nne YA mwaka2012.



0 comments:

Post a Comment