Msanii
maarufu kutoka Tanzania anaefanya vizuri katika Tasnia ya muziki wa
bongo Fleva Nchini na Nje ya mipaka ya Tanzania Ambwene Yesaya
alimaarufu kama AY.
AY
anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la JIPE SHAVU
aliompa shavu msanii Fid Q kutoka pande za Rock City Mwanza vilevile
wimbo huo umetengenezwa katika studio Mpya itwayo Mpo Afrika chini ya
Producer Q.
“Ijumaa
naachia wimbo wangu mpya huo nilioufanya na Fid Q baada ya kukamilika
hivyo mashabiki wakae tayari kwa wimbo huop ijumaa hii”alisema AY
AY
anatarajia kuachia wimbo wake lakini mwezi uliopita msanii huyo
alishirikiana na Mwanafalsafa MWANA FA pamoja na J Martin kutoka
Nigeria na kutengeneza wimbo waliosema ungetoka mwishoni wa mwezi wa
nne au mwanzoni wa mwezi huu wa tano baada ya kufanya Kichupa cha
Wimbo huo.
0 comments:
Post a Comment