10:00 PM
NG’OMBE – TAURUS (APR21
– MAY 20)
Leo Watu hawa watakusaidia sana na hiyo ni dalili ya
mambo yako kukunyookea na kupata vitu ulivyokuwa unavihitaji kwa muda
mrefu. Ili kuleta baraka nenda Kanisani au Msikitini.
MAPACHA
- GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Huko uendako hakuna maeleweno ni bora
ukajirudia zako nyumbani ili kuepusha shari la bure. Katika kipindi
cha siku tatu kutoka leo unaweza kupata habari nzuri. Kila jambo lako
linapokutatiza peleka shauri lako kwa mzee wako Mwanamume au mjomba
wako
KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Mwezi huu madeni
uliyonayo yanakupa matatizo na hali yako ya kimaisha imebadilika
sana, hiyo ni mitihani na dalili za mafanikio katika mambo yako
zitaanza kuonekana baada ya siku kumi na nne, unashauriwa kama una
mipango iwe kabla ya mchana au baada ya jua kuzama.
SIMBA –
LEO (JUL 24 – AUG 23)
Leo una wasiwasi mwingi, vile vile kifua
kinakuuma hiyo ni dalili ya kuharibikiwa kwa mipango yako na
usipokuwa makini unaweza ukajikuta unapoteza vitu vya thamani kubwa
kizembe.kuwa muangalifu.
MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT
23)
Mchana huu kuna balaa linakusakama na Unataka sana utoke
katika Balaa kama hilo. Muone m,zee wako na muelezee matatizo yako
atakupa ushauri ambao utakusaidia sana.
MIZANI – LIBRA
(SEPT 24 – OCT 23)
Leo bahati itakujia, furaha au barua au
habari unazozitarajia utapata Mchana huu Jaribu sana kuwa makini
unaweza kupoteza fedha kwa kutapeliwa na mtu wako wa karibu.
NGE
- SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Mambo yako unayoyataka yote yatakuja
kwa sharti kwamba lazima upate msaada wa mtu, unashauriwa kuwaona
wataalamu ili kukinga hali mbaya isitokee, ukidharau unaweza kufungwa
au kupoteza mtu.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Leo
utakutana na mtu na lazima umuonyeshe na kumueleza kuwa hali yako ni
mbaya na ya wasiwasi atakusaidia. Wiki hii utatukuzwa kwa jambo
utakalolifanya na utapata mafanikio katika malengo yako uliyoyapanga
hapo nyuma.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Mwezi
huu utashirikishwa katika mazungumzo ya kibiashara ambayo
yatakupeleka sehemu nzuri na za kukufurahisha. Hata mkikubaliana na
huyo mshirika wako katika biashara lazima ujue atakuambia ungoje
kidogo au kukucheleweshea mahitaji yako lakini baadae utaokoka.
NDOO
–AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Katika maisha yako utasaidiwa
sana na mtu aliyezaa mtoto wa kiume au baada ya wewe kuzaa mtoto wa
kiume. Mambo yako yako karibu kufunguka hasa ukipata habari ya
kuzaliwa mtoto.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo
utapata bahati nzuri, changamkia shughuli nyingi za kifedha au
kibiashara, kwani mambo yako yatakuwa yanakwenda haraka haraka
kinyume na ulivyotegemea. Ukipata pesa zitumie katika mambo ya maana.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Unashauriwa wiki hii kwa
ajili ya kufuzu haja yako lazima ufuatane na mtu aliezaa au ufuatane
na mtoto wa kiume mdogo utaona ajabu. Utajionea mambo ya kuchekesha
na kufurahisha sana, kuwa mtulivu zaidi hasa nyakati za jioni.
imendaliwa na Mtabiri Maalim Hassan
0 comments:
Post a Comment